Kijana ambaye ni dereva wa toroli la miguu minne jina lake
halikuweza kupatikana mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32
amefariki dunia papo hapo na kupasuka Kichwa baada ya kugongwa na basi la
abiria lililokuwa likitokea mkoa wa Geita kuelekea jijini Mwanza kwenye
makutano ya barabara ya Kamanga na Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Kijana huyo pia alikuwa akiendesha Pikipiki bila kuvaa “Helmet” huenda
ingemsaidia asipasuke Kichwa.(Picha na Zainul Mzige).
Na MOblog, Sengerema
Mtu mmoja ambaye hakutambulika jina lake mara moja
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38
(mwanaume) kufa papo hapo Na wengine wawili kujeruhiwa baada
ya kugongwa na gari kwenye makutano ya barabara ya Kamanga na Busisi wilayani
Sengerema mkoani Mwanza.
Tukio hilo limetokea jana Juni 30 majira ya saa 9 alasiri
ambapo basi la abiria mali ya kampuni ya Lushanga lenye namba za usajili T 312
ATA likiwa na Abiria likitokea Mkoa wa Geita kuleleka mkoani Mwanza kupitia
kivuko cha Kamanga.
Marehemu alikuwa anaendesha troli lililokuwa limebeba miti
ambapo amepasuka kichwa na kusababisha Ubongo kutoka nje, na mwili wake
umepelekwa katika hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya uchunguzi
zaidi pamoja na majeruhi kwa ajili ya matibabu.
Baadhi ya wakazi wa Sengerema wakijaribu kutoa huduma ya
kwanza kijana mwingine aliyepasuka eneo la jichoni baada ya ajali hiyo kutokea.
Kijana huyo alionekana kuchanganyikiwa pamoja na maumivu makali baada ya
kutokea ajali hiyo.
Kwa upande wa mashuhuda abiria waliokuwa katika basi hilo
hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo pamoja na gari hilo kuharibika baada ya
kushindwa kuendelea na safari hivyo kurudi nyuma na kujikita kwenye mtaro.
Hadi tunaandika habari hii chanzo cha ajali hii
hakijajulikana kutokana na uchunguzi wa polisi wilayani humo kuhusu ajali hiyo
kuendelea na dereva wa basi hilo na konda wake waliotokomea kusikojulikana
kutokana na mkusanyiko wa watu eneo la tukio.
Tutakuletea taarifa zaidi baada ya Polisi kutoa ripoti ya
chanzo cha ajali hiyo.
Raia wema wakijaribu kumtuliza mmoja wa majeruhi alale chini
kwa muda kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kuasuka eneo la karibu na jicho lake huku mwendesha Baiskeli naye akiwa
amepoteza fahamu kwa muda.
No comments:
Post a Comment