Rais Jakaya Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji
kwa upande wa Wilaya ya Nachingwea katika Kijiji cha Chiumbati mkoani Lindi. Mradi huo
mkubwa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 pia unajumlisha Wilaya ya Masasi iliyopo
Mkoa wa Mtwara. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Prof Jumanne
Magembe, na kushoto ni Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chiumbati wilayani Nachingwea
baada ya kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji kwa
upande wa Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Mradi huo mkubwa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 pia unajumlisha Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Kushoto aliyekaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifuatiwa na Waziri wa Maji, Prof Jumanne Magembe.
upande wa Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Mradi huo mkubwa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 pia unajumlisha Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Kushoto aliyekaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifuatiwa na Waziri wa Maji, Prof Jumanne Magembe.
Rais Jakaya Kikwete akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Nachingwea mjini mara baada ya
kuzindua mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 unaojumlisha Wilaya
ya Nachingwea na Masasi mkoani Mtwara. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifuatiwa na Waziri wa
Maji, Prof Jumanne Magembe.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe akimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji jimboni
kwake Nachingwea mkoani Lindi. Mradi huo wa Maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6
unajumlisha Wilaya ya Nachingwea na Masasi iliyopo Mkoa wa Mtwara. Katika hotuba yake
fupi ya kumshukuru Rais Kikwete, Waziri Chikawe alisema jimbo lake lilikuwa linateseka
na shida ya maji kwa kipindi kirefu lakini sasa tatizo hilo limekwisha. Picha zote na Felix
Mwagara wa WMNN.
No comments:
Post a Comment