Diwani aliyesimama Bi. Twilumba Wapalila enzi za uhai wake akiendelea na majukumu yake
kama mwakilishi wa wananchi.
Diwani wa kata ya
Lupembe wilayani Njombe Bi Twilumba Wapalila, amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipata matibabu katika hospitali ya
Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika zilizopatikana kutoka kwa viongozi kabla ya kuanza kwa kikao
cha baraza la madiwani la Halmashauri ya
Wilaya ya Njombe wamesema kuwa hii leo
watalazimika kufupisha kikao kutokana na msiba huo.
Aidha Baadhi ya wajumbe hao licha ya kuonekana kuwa na
simanzi lakini pia wamebainisha kuwa
marehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Msiba huu ni wa pili kwa tarafa ya Lupembe na wa tatu kwa
Chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe kufuatia siku chache zilizopita aliyekuwa
diwani wa kata ya mfiliga kufariki ikiwa
ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama
Hicho Marehemu Adam Msigwa.

No comments:
Post a Comment