Dunia imekwisha! Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia
mtoto wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la sita kwa tuhuma
nzito ya kuwalawiti wenzake watano kwa mpigo.
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Twanga Pepeta, Kitwana Tupa.
Mwanahabari wetu alifunga safari hadi kijijini hapo ambapo
baadhi ya wananchi waliohojiwa walidai kwamba dogo huyo alikuwa akiwalawiti
wenzake kwa kigezo cha kuwapanga kwenye mechi za mpira wa matambara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Poul.
lli kupata undani wa tukio hilo, mwanahabari wetu alifika
nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kukuta tayari jeshi la polisi lilifika
limeshamkamata.
Mjumbe wa serikali ya mtaa huo wa Twanga Pepeta Kitwana Tupa
alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanasubiri sheria ichukue mkondo wake
baada ya kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Poul.
No comments:
Post a Comment