![]() |
| PICHA NA MAKTABA |
Dar es Salaam. Wakati wanawake kwa wanaume wengi huenda
barani Asia, hasa China kununua bidhaa kwa ajili ya kuja kuzichuuza, hali sasa
ni tofauti kwa kuwa kuna wasichana ambao huenda huko kwa ahadi za ajira, lakini
huishia kufanya ukahaba kwenye madanguro, gazeti hili linaweza kukuthibitishia.
Wasichana hao hutafutwa na mawakala wa hapa nchini ambao
kazi yao huwa ni kutafuta wasichana wazuri na baadaye kuwashawishi kwa
kuwaeleza fursa za ajira za hotelini zilizo barani Asia.
Msichana akikubali, wakala huchukua jukumu la kumtafutia
viza ya kuingia China na baadaye kuwasiliana na mwenyeji wake, maarufu kama
Lady Boss, ambaye hutuma tiketi ya ndege kwa ajili ya kumsafirisha ‘mwajiriwa’
mpya.
Hata hivyo, hali hubadilika mara wafikapo huko kwa kuwa
‘mwajiri’ huyo humpokonya hati ya kusafiria na baadaye kumpa maelekezo kuwa
atatakiwa kulipa Dola 200 kila siku ambazo atakuwa akizipata kwa kufanya
umalaya kwenye klabu na maeneo ya biashara.
Tayari wasichana kadhaa wa Kitanzania wamenaswa katika mtego
huo na kujikuta wakilazimika kuuza miili yao ili wamudu ada ya Dola 200 pamoja
na fedha za kujikimu, akiwemo Munira Mathias mwenye umri wa miaka 23 ambaye
alimudu kuvaa ujasiri wa kuweka bayana uovu huo katika mazungumzo yake na
gazeti hili.
Binti huyo Mtanzania aliyesafiri kwa saa 18 kwenda Guangzou,
China alitakiwa kupumzika kwa saa mbili tu kabla ya kupelekwa kuanza ‘kazi’
ambayo hakuitarajia.
“Baada ya kupumzika kwa saa mbili tu, nilipelekwa kwenye
klabu,” anasema Munira wakati akisimulia mkasa wake.
“Sikuwa na kazi
nyingine zaidi ya kucheza muziki na wanaume ambao licha ya kwamba sikuwahi
kuwaona, walinichangamkia kama vile wananifahamu.”
Munira aliondoka Januari mwaka huu kwenda China ambako
aliahidiwa kuwa angeajiriwa hotelini, lakini alikutana na ‘ajira’ ya ukahaba,
huku akilazimika kuwalipa ‘waajiri’ wake Dola za Marekani 200 kila siku.
Binti huyo, ambaye
alifanikiwa kuchomoka mikononi mwa waajiri hao baada ya viza yake kuisha,
alisema kwa siku 91 alizokaa China, alipata mateso ambayo hatayasahau ikiwamo
kupigwa, kubakwa na kundi la wanaume raia wa Nigeria, pia kulazimika kutoa
mimba aliyoipata kwa kubakwa.
“Nilifika Guangzhou
kama saa 9.00 alasiri za China na kulikuwa na baridi sana,” anasema Munira
akisimulia jinsi alivyokanyaga kwa mara ya kwanza ardhi ya nchi hiyo akiwa na
matumaini ya kuanza maisha mapya.
“Wakati huo nilikuwa nikijaribu kupata mawasiliano na
mwenyeji wangu ambaye niliagizwa kutoka Magomeni, Dar es Salaam.Chanzo MwanaincHi


No comments:
Post a Comment