Stori: Mwandishi Wetu
Za mwizi arobaini! Ule mchezo wa kukwapua vitu na kukimbia
umemtokea puani dereva wa pikipiki almaarufu bodaboda aliyetambulika kwa jina
la Abuu Athumani (28) ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu ya bei mbaya
ya mrembo aitwaye Zaituni Hamisi.
Dereva wa bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani
ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu.Tukio hilo la aina yake lilijiri
majira ya asubuhi wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa…
Dereva wa bodaboda akiwa kwenye mtaro na pikipiki yake mara
baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.
Shuhuda huyo alisema kuwa alishangaa kumuona yule jamaa
aliyepakizwa akimkwapua mrembo huyo lakini kwa bahati nzuri mmoja wa madereva
wa Bajaj aliyekuwa karibu alimuona na kumbananisha pembezoni mwa barabara na
hatimaye kuingia mtaroni.
Zaituni Hamisi (kulia) aliyekwapuliwa simu yake na waendesha
bodaboda.
Alisema ghafla umati ulijaa na kushuhudiwa akipewa kipondo
cha kufa mtu na wengine wakidai kuwa ni kawaida ya jamaa huyo kukwapua mikoba
ya watu.Baadhi ya watu walikuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kununua mafuta ya
petroli ili wamchome moto bila kujali polisi aliyefika ambaye alikuwa
akijitahidi kutuliza ghasia hizo.
Dereva huyo wa bodaboda akichukuliwa na Polisi mara baada
kunusullika kifo kutoka wa wananchi.
Wakati akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na
kuwaomba wananchi wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda
huyo alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika
eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua za
kisheria.
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Jamila Said na Deogratius
Mongela.
No comments:
Post a Comment