MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kanda ya kusini ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Avangelisitic Assemblies of God
Tanzania(EAGT),Joseph Matare amejiuzulu
nafasi yake hiyo kutokana na Kanisa lake hilo Kuagiza Wachungaji wake ambao ni
Viongozi wa Vyama vya Siasa kuachana na
Nafasi zao za Kisiasa.
Joseph Matare
akizungumza na Waandishi wa habari Mjini Songea amesema kuwa ameamua kujuzulu
Nafasi yake ya Uongozi wa CHADEMA Kanda
ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma kufuatia Kanisa lake katika Mkutano wake wa Kanda kuagiza Wachungaji wake
wote ambao ni Viongozi wa Kisiasa kuachia nafasi zao na badala yake wasimamie
Kazi ya Mungu Katika Makanisa yao.
‘Kufuatia
maagizo ya Mkutano huo wa Kanisa
uliofanyika Njombe nimeamua kutii na leo
tarehe 10 Julai 2014 nimeamua
kujiuzulu na Katibu wangu Mkuu Dr Wilbroad Slaa
nilimjulisha tangu tarehe 04 Juni mwaka huu’ alisema Matare katika taarifa yake ya kujiuzulu.
Anafafanua kuwa
muda wa Viongozi wa Kanda ulikuwa ni wa
muda na wa mpito hadi uchaguzi wa Kanda
utakapopita ambao ulipaswa kufanyika
Juni 2014 na kwamba muda umeongezwa hivyo ameona aheshimu maagizo yaliyomuweka madarakani.
Hata hivyo Matare
anasema kuwa anawatia moyo Makamanda wote wa CHADEMA waliobaki kuendelea kupigania Nchi ili
iondokane na uovu unaotendeka sasa na
kwamba Mungu atakuwa nao wale wote wanaotafuta haki kwa ajili ya Wananchi walio
wengi.
Anasema kuwa ameondoka bila kuwa na Ugomvi na
Kiongozi yeyote wa CHADEMA hivyo
wataendelea kushirikiana kutafuta haki
akiwa Mwanachama wa Kawaida na Mchungaji.
Matare ambaye ni
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mkuzo la
Mjini Songea la Mkoani Ruvuma amesema
kuwa anatambua juhudi za Viongozi wa CHADEMA katika kupigania haki za Wananchi
na Wabunge wote wa CHADEMA katika kupigania haki na kwamba ipo siku Mungu
atawalipa ujira wa kazi wanayofanya.
Anasema kuwa Mungu
anatambua kazi nzito wanayofanya Viongozi
wa CHADEMA ambayo amesema ni ya kutafuta Ukombozi kamili wa Nchi na
itakuwa ni uendawazimu kubeza kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment