skip to main |
skip to sidebar
HUYU NDIYE REFA ATAKAYECHEZESHA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA JUMAPILI
Nicola Rizzoli amechaguliwa na Fifa kuwa
mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia Brazil 2014 kati ya
Ujerumani na Argentina.
Howard Webb kutoka England, aliyechezesha fainali ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, aliorodheshwa lakini hakuchaguliwa.
Ujerumani itapambana na Argentina kwenye dimba la Maracanã, jijini Rio De Janeiro, siku ya Jumapili Julai 13.
Rizzoli ni msanifu majengo kutoka Bologna, na tayari amechezesha mechi tatu katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 42 alichezesha mechi kati ya Spain
dhidi ya Uholanzi, Nigeria na Argentina na Argentina ilipocheza na
Ubelgiji.
Rizzoli pia alichezesha mchezo wa fainali ya Ligi ya
Europa kati ya Atlètico Madrid dhidi ya Fulham mwaka 2010, na pia mchezo
wa fainali ya Uefa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2013 kati ya Bayern Munich
na Borussia Dortmund.
Rizzoli atasaidiwa na waamuzi wa pembeni
Renato Faverani na Andrea Stefani, na mwamuzi wa nne atakuwa Carlos Vera
kutoka Ecuador.
Rizzoli atakuwa mwamuzi wa tatu kutoka Italy
kuchezesha fainali, baada ya Sergio Ginella mwaka 1978 na Pierluigi
Collina mwaka 2002
No comments:
Post a Comment