Tarehe
1 Juni 2014 tuliondokewa na Mama yetu mpenzi Bi. Shida Salum. Mauti
yalimkuta mama katika Hospitali ya AMI, Masaki jijini Dar es Salaam na
mazishi kufanyika mjini Kigoma mnamo tarehe 2 Juni 2014.
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote
walioshiriki nasi katika msiba huu mkubwa kwetu. Tunawapa shukrani zetu
madaktari na wahudumu wa Hospitali za Muhimbili,
Apollo (Cancer and Main) jijini Chennai nchini India na AMI jijini Dar
es Salaam kwa juhudi zao kubwa za kumhudumia mama yetu. Tunatoa shukrani
kwa Imam wa Msikiti wa Maamur Dar es Salaam na Sheikh wa Mkoa Kigoma
Alhaj Hassan Kiburwa kwa ibada ya maiti.
Tunatoa shukrani zetu
za dhati kwa Uongozi mzima wa Bunge Maalum la Katiba, Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mkoa wa Kigoma na Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Serikali kwa ushirikiano mkubwa waliotupa katika mtihani
mkubwa uliotufika. Tunashukuru wote waliofika Kigoma kwenye mazishi na
wale waliotuletea salaam za rambirambi. Mwenyezi Mungu atawalipa kheri
na kuwafanyia wepesi, Inshaallah.
Ibada ya 40 (Hitma) ya mama
itafanyika nyumbani kwake Tabata Bima (Flats za NSSF) jijini Dar es
Salaam siku ya Jumamosi tarehe 12 Julai, 2014 kuanzia saa Kumi na Moja
jioni (kabla na baada ya sala ya Magharibi).
INNA LILLAH WAINA ILAIH RAAJIUN
TANZANIA NA OMAN ZAIMARISHA USHIRIKIANO USIMAMIZI KUMBUKUMBU NA NYARAKA
KIDIJITALI
-
Na. Jawadu Kinyobwa – Dar es salaam
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea vifaa vya kisasa vya
Chumba cha Kanzi Data, vifaa vya Teknolojia...
1 hour ago


No comments:
Post a Comment