Watu wakiuangalia
mwili wa mtu ambaye hakufahamika jina jina lake baada kugongwa na gari
lisilofahamika na kufa papo hapo, katika eneo la bohari ya mkoa kati ya bunge
na kituo cha mabasi yaendayo mikoani, barabara ya Morogoro - Dodoma.
Polisi wa usalama barabarani wakisaidiana na wananchi
kuupakia mwili wa mtu aliyekutwa amegogwa na kufa papo hapo na gari ambalo halikujulikana
baada ya kukimbia katika barabara ya Morogoro - Dodoma karibu na jengo la bunge
la Tanzania.
Na John Banda, Dodoma
MWANAMKE asiyefahamika wa umri wa makamo amepoteza maisha
baada ya kugongwa na gari aina ya Coster linalofanya shughuli za Daladala kati
ya Udom Nanenane ambalo halikufahamika namba zake za usajili na kisha Gari hilo
kutokomea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa mashuhuda walioshudia tukio hilo wamesema
majira ya saa 2. 30 walishuhudia kishindo kikubwa Barabarani eneo la Bohari
karibu na kipitashoto kilichopo kituo cha mabasi yaendayo mikoani mjini Dodoma,
ambapo baada ya kishindo hicho gari hilo liliendelea na safari zake. Mmoja wa
mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Baraka amesema hakumuona mtu
huyo wakati anavuka bali aliona Costaer hiyo mita chache kabla ya kusikia
kishindo hicho na kilichomfanya ajue kuwa
ni mtu kagongwa ni kutokana na gari la nyuma kumulika mwanga
ndipo alipoona tairi ya nyuma ikimalizikia kumkanyaga na kufa hapohapo.
Mkaguzi wa polisi wa usalama Barabarani Methew Mtakije aliyefika kushuhudia tukio hilo alisema tukio
hilo lilisababishwa na mwendo kasi wa Dereva wa gari hilo ambaye alikiuka
sheria za usalama barabarani ambazo zinamtaka kila dereva kuendesha spidi 50
kwa saa wanapokuwa
mijini.
MtakijaAmesema mwendo kasi ni hatari wakati wowote hasa nyakati za usikukutokana
na muono mdogo unaosababishwa na giza hivyo madereva wotewazingatie sheria
zilizopo ili waweze kuepusha ajili, na kuahidi kulisakagari hilo mpaka
kulipata. Mwili wa Marehemu huyo ambae bado hajafahamika umehifadhiwa katika
chumba cha maiti kilichopo katika hospitali yamkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment