Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma
Sehemu ya Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma..(picha na Freddy Maro).
Julai,2014
Saidieni watu kutoka kwenye umasikini,
Rais awaagiza viongozi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezitaka taasisi
za Serikali kuongeza kasi ya kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi, akisisitiza
kuwa wananchi wamekaa katika umasikini kwa muda mrefu mno kupita kiasi.

Kikwete amesema kuwa wanachotarajia wananchi kutoka kwa taasisi za Serikali ni kusaidiwa
kutoka kwenye umasikini kwa kasi kubwa zaidi kwa sababu wamekaa katika hali ya umasikini
kwa muda wa kupita kiasi.

Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumapili, Julai 20, 2014, wakati alipokagua shamba
la kisasa la zao la buni kwenye kijiji cha Lipokela, Wilaya ya Songea, ikiwa ni
moja ya shughuli zake katika siku ya nne ya ziara yake ya siku sita katika Mkoa
wa Ruvuma.

Kikwete amesimama kwenye shamba hilo akiwa njiani kutoka Wilaya ya Mbinga kuelekea
Wilaya ya Songea ambako leo amefungua soko la kimataifa katika kijiji cha
Mkenda, kilicho mpakani kabisa mwa Tanzania na Mozambique. Baadaye, Rais amekagua
daraja kwenye Mto wa Ruvuma ambalo linaunganisha Tanzania na Mozambique.

Kikwete ametoa maelekezo hayo baada ya kuambiwa kuwa pamoja na kwamba shamba hilo,
pengine ni kubwa kuliko jingine lolote la buni nchini, limefanikiwa kupata miche
3,000,000 ya buni za kisasa ambayo lilihitaji lakini wakulima wa kawaida wa zao
hilo la kahawa wanashindwa kupatiwa kiasi hicho hicho cha miche ya buni.

“Kwanini
tunashindwa kupata miche milioni tatu kwa ajili ya wananchi ambayo wenyewe mmesema
kuwa gharama yake yak uizalisha ni shilingi milioni 900? Kwanini tunashindwa kupata
miche ya kutosha ili wakulima wetu wapande na kuongeza kipatoc hao?”Rais
Kikwete amemwuuliza Profesa James Teri, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Kahawa
Tanzania (TACRI).

Ameongeza
Rais Kikwete: “Hatuwezi kuwabakiza wananchi wetu katika umasikini kwa miaka mingine
30 kwa sababu tu hatuna uwezo wa kuzalisha miche ya kutosha. Hatuwezi kufanya hivyo,
wameishi kiasi cha kutosha katika umasikini.”

Amesisitiza
Rais Kikwete: “Kazi yetu ni kuwatoa watu wengi zaidi katika umasikini kwa haraka kubwa
zaidi kwa sababu wamechelewa mno. TACRI inaweza kufanya hivyo kwa kuwapa wananchi
mbegu bora zaidi ya buni, ili waondokane na mibuni ya zamani ambayo uzalishaji
wake ukochini. Hivyo, nataka kujua tunaweza kufanya nini kufanikisha hili siyo kuniambia
habari ya changamoto ambazo TACRI inakumbana nazo katika kutimiza majukumu yake.”

Rais Kikwete: “Siridhiki na kasi ya kujaribu kuwatoa watu wetu katika umasikini.
Nahitaji kupata miche milioni tatu kwa ajili ya wananchi wetu. Kama iliwezekana
kulipatia shamba hilo miche milioni tatu kwa nini isiwezekane kwa wananchi?”

Shamba hilo kubwa la mibuni
(inayozalisha kahawa) ni mali ya Kampuni ya AVIV, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni
ya Olam International, ambayo inaendesha shughuli za biashara katika nchi 65
duniani.

Olam
iliingia Tanzania miaka 20 iliyopita na shughuli zake kubwa ni katika mazao ya korosho
na kiwanda cha kuchambua pamba kilicho Bunda, Mara.

Duniani,
Olam ina mashamba ya mibuni katika nchi tano ambazo ni Tanzania, Zambia,
Ethiopia, Laos na Brazil.

AVIV
ambayo inapanda mibuni ya kuzalisha kahawa yaa ina ya Arabica ilipanda miche ya
kwanza miaka mitatu iliyopita na inakaribia kuvuna kwa mara ya kwanza. Katika kijiji
hicho cha Lipokela, AVIV ina ardhi yenye ukubwa wa hekta 2,000.Rais
Kikwete anaendelea na ziara yake katikaMkoa wa Ruvuma leo kwa kutembelea na kukagua
shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Namtumbo.

Imetolewa
na;
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
20Salaam.
Julai,2014
No comments:
Post a Comment