Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 9, 2014

MIROSLAV KLOSE AVUNJA REKODI NA KUWA MFALME WA MABAO KOMBE LA DUNIA


Mvunja rekodi: Miroslav Klose ni mfungaji bora katika historia ya kombe la dunia.
Miroslav Klose amevunja rekodi ya Ronaldo na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya fainali za kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo wa Ujerumani alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia na kufikisha mabao 16.
Lilikuwa bao lake la pili katika mashindano baada ya kufunga bao akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Ghana,  hatua ya makundi na kumfanya alingane mabao na gwiji wa Brazil.


 Historia: Shuti lililomfanya ashikilie rekodi ya dunia

WAFUNGAJI  WA JUU WA KOMBE LA DUNIA

Miroslav Klose 16 goals
Ronaldo 15
Gerd Muller 14
Just Fontaine 13
Pele 12
Jurgen Klinsmann 11
Gary Lineker 10
Klose alicheza kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia mwaka 2002 na kufunga mabao matatu `hat-trick` katika ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya  Saudi Arabia.

Alifunga tena bao katika 


mechi iliyofuata ya makundi ambayo Ujerumani ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Jamhuri ya  Ireland, kabla ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Cameroon.

Licha ya Ujerumani kufika fainali mwaka ule, Klose alishindwa kufunga tena katika mashindano, akimaliza michuano kwa idadi sawa ya mabao na Rivaldo, nyuma ya mfungaji bora, Ronaldo aliyefunga mabao 8.

Miaka minne baadaye, Ujerumani walikuwa wenyeji wa fainali za dunia (2006), mshambuliaji huyo alifunga mabao matano tena ambayo yalitosha kumpatia kiatu cha dhahabu.

No comments:

Post a Comment