Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 16, 2014

NANE WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI KAGERA


Polisi  mkoani Kagera inashikilia watu wanane kwa tuhuma za mauaji yaliyofanyika  Wilaya za Bukoba na Missenyi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Henry Mwaibambe alisema kuwa matukio hayo yalitokea Juni 14 mwaka huu.
Tukio la kwanza lilitokea Katika kijiji cha Ibaraizibu kata ya Karabagaine Bukoba Vijijini ambapo mtu mmoja aliuawa na walinzi wa kampuni ya Shoes
Shine Guard Security (SGS) ambao walikuwa wakilinda chuo cha kilimo Maruku.
Mwaibambe amesema Polisi inawashikilia  walinzi Adroph Simula (55), Marco Sita (27), Deus Kato (34) na Godfrey Alexander (27).
Imedaiwa kwamba walinzi hao waliacha 

 
kituo chao cha kazi usiku wa manane katika kata  ya Maruku Bukoba Vijijini na kwenda kuvamia nyumbani kwa Felix Alexander (40-45) mkazi wa Ibaraizibu Bukoba Vijijini na kumteka kisha wakampeleka mpaka chuoni kwao na kuanza kumshambulia kwa fimbo na kitu chenye ncha kali kichwa na kilichosababisha kufa papo hapo.
Alisema baada ya mauaji hayo, raia wema walipiga simu polisi ambapo polisi walifika na kuwakamatwa walinzi hao na baada ya kuhojiwa walijibu kuwa mapema mwezi Juni mwaka huu, marehemu alifika katika chuo hicho na kuvunja kisha akaiba mashuka, televisheni na samani mbalimbali
ambavyo vilikuwa nyumbani kwa marehemu lakini hawakuwahi kutoa taarifa yoyote kituo cha polisi.
Tukio la pili lilitokea katika kijiji cha Karora Kata ya Kakunyu Wilayani Missenyi ambapo wananchi walivamia kitalu namba tatu cha ufugaji kilichomilikishwa kwa mwekezaji aitwaye Sosoma Shimula na kumuua mlinzi wa kitalu hicho aitwaye Mwemezi Cosmas maarufu kama Barungula (32).
Mwaibambe alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 14 majira ya saa tano asubuhi ambapo wananchi ambao ni wafugaji wakiwa na mifugo yao walivamia katika kitalu hicho kwa lengo la kulisha mifugo yao ambapo mlinzi  Cosmas wa kampuni ya Nyamihaga Security aliwazuia kuingiza mifugo yao katika eneo hilo lakini walikaidi na kuanza kumshambulia kwa visu, mapanga na fimbo mpakamauti ikamfika mlinzi huyo.
Alisema wakati wakiendelea na uovu huo baadhi ya wananchi walipiga simu polisi Missenyi ambapo walifika na kuwakamata wananchi wanne wenye asili za nchi za Rwanda na Uganda ambao ni wachungaji wa ng’ombe katika kijiji cha Karora.
Kamanda aliwataja watu hao kuwa ni Terejea Bazambaza (17) Mnyankole, Nchundizena Kasinzi (27) Mnyarwanda, George Kagusaga (27) na Ndyezeya Mwemezi (30) Mnyankole.

No comments:

Post a Comment