Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 27, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MAHAFALI YA KOZI YA PILI YA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI TAASISI MALUUM UTOAJI MAFUNZO YA USALAMA WA KITAIFA NA KIMATAIFA

Profesa ibrahim lipumba akisalimiana na mkuu wa majeshi ya ulinzi  David Mwamunyange wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha jeshi  NDC

MKUU WA JESHI LA POLISI  MANGU AKIWA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MECK SADIK

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGEA NA WAKUU WA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA



RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA ERNEST WAMBA DIA WAMBA

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIFURAHIA JAMBO PAMOJA NA DR BANA NA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA
WAHITIMUWA JESHI




RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAHITIMU WA MAHAFALI

RAIS AKIWA NA WATU MBALIMBALI

WAHITIMU WA CHUO CHA JESHI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

RAIS JAKAY KIKWETE AKIELEKEA KATIKA JUKWAA

RAIS AKIONGEA NA BAADHI YA MABALOZI

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIAGANA WAKUU WA JESHI LA ULINZI

RAIS JAKAY KIKWETE AKIELEKEA KATIKA JUKWAA 

BAADHI YA WANAJESHI WAHITIMU KATIKA CHUO CHA JESHI WAKATI WA MAHAFALI YA PILI YA CHUO HICHO

BAADHI YA WANAJESHI WAHITIMU KATIKA CHUO CHA JESHI WAKATI WA MAHAFALI YA PILI YA CHUO HICHO 

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWAAGA WAHITIMU WANAJESHI WA CHUO CHA JESHI LEO

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIFURAHI KITUPAMOJA NA WAGENI MBALIMBALI
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam . Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam . Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam .Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam


PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment