Watu sita jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma wakikabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kujihusisha na biashara ya kusafirisha na kuuza meno ya tembo ambapo walikamatwa wakiwa na vipande 18 vya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 228.8.
Washtakiwa hao wametajwa kuwa ni Mwinyi Igonza, Lucas Mayai, Emmanuel Sindano, Daud Mwaja, Yohana Chamaulaya na Juma Malyango.
Wakili wa Serikali Godfrey Wambali alidai mbele ya Hakimu Mkazi Rhoda Ngimilanga kuwa katika mashtaka ya kwanza washtakiwa wanadaiwa kujihusisha na biashara ya nyara za serikali.
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2002 hadi Juni 13 mwaka huu katika Mkoa wa Dodoma, washtakiwa kwa pamoja
walikuwa wakijihusisha na biashara ya kusafirisha na kuuza meno ya tembo ambapo siku ya tukio walikamatwa wakiwa na vipande 18 vya meno ya tembo yenye uzito wa kilo 326.5 vyenye thamani ya Sh milioni 228.8 mali ya Serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Katika mashtaka ya pili ilidaiwa washtakiwa walikuwa wakimiliki nyara za serikali bila kuwa na uhalali. Ilidaiwa mahakamani kuwa Juni 13, mwaka huu katika Kijiji cha Ilangali Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma washtakiwa kwa pamoja walikamatwa wakimiliki nyara za serikali ikiwa ni vipande 18 vya meno ya tembo mali ya Serikali. Pia wanadaiwa kuongoza kundi la uhalifu.
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari mosi mwaka 2002 na Juni 13, mwaka huu washtakiwa kwa pamoja waliongoza kundi la uhalifu kwa kukusanya na kuuza vipande 18 vya meno ya tembo mali ya Serikali.
Washtakiwa walikana mashtaka yao na kupelekwa rumande baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Elieza Feleshi kuwasilisha hati mahakamani ya kupinga dhamana yao kutokana na kesi hiyo kuwa na maslahi ya umma. Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Julai 29, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment