Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 11, 2014

TAZAMA PICHA 8 ZA MAN CITY WAKIKWEA PIPA KWENDA SCOTLAND KUWEKA KAMBI YA MAANDALIZI YA MSIMU


Tabasamu kubwa: Mshambuliaji wa Man City ambaye hajatulia , Alvaro Negredo akicheka wakati alipokuwa anapenda ndege kwenda Dundee.

KIKOSI cha mabingwa wa England, Manchester City kimekwea pipa kwenda Dundee tayari kuanza ziara yao ya maandalizi ya msimu huko Scottish.

Katika msafara huo, pia umemjumuisha mshamabiliaji ambaye hajatulia kwa sasa, Alvaro Negredo aliyeonekana kuwa katika morali nzuri.

Kikosi cha Manuel Pellegrini kitacheza Dundee siku ya jumapili kabla ya kusafiri siku inayofuata kwenda Edinburgh kucheza dhidi ya Hearts siku ya ijumaa.

Negredo anayehusishwa kuondoka Etihad, alipigwa picha akipanda ndege binafsi ya Man City, `City Jet` jana jioni, huku naye kipa mpya, Willy Caballero akiwemo katika msafara huo.


Big bosi!: Kocha wa City, Manuel Pelligrin atakuwa na kikosi chake nchini Scotland na baadaye atakwenda  America.

Kifaa kipya: Kipa mpya wa Man city, Willy Caballaro pia yumo katika msafara wa klabu hiyo kwenda nchini Scotland kufanya maandalizi ya kabla ya msimu.




No comments:

Post a Comment