Algeria imesitisha shughuli za kandanda kwa kipindi
kisichofahamika kufuatia kifo cha mchezaji kutoka Cameroon, Albert Ebosse
aliyekufa baada ya kurushiwa kitu na mashabiki. Shirikisho la kandanda la
Algeria limefikia uamuzi huo siku ya Jumapili. Ebosse, 24, aligongwa na kitu
kichwani wakati akitoka
uwanjani baada ya mechi kumalizika kati ya timu yake JS
Kabylie iliyofungwa na USM Alger siku ya Jumamosi, jijini Tizi Ouzou. Mamlaka
za Algeria awali zilikuwa zimeufungia uwanja wa Novemba Mosi 1954 lilipotokea
tukio hilo. Amri hiyo sasa inajumuisha viwanja vyote nchini humo. Shirikisho
hilo pia limesema litatoa dola 100,000 kwa familia ya Ebosse, kiasi ambacho
angelipwa katika muda wa mkataba wake. Zaidi ya hilo, wachezaji wa JS Kablylie,
kila mmoja atatoa mshahara wa mwezi mmoja.
No comments:
Post a Comment