Sony imefunga mtandao wa Playstation
Katika ujumbe kwenye mtandao wake , Sony imesema kuwa hakuna
habari za watu binafsi zilizohatarishwa kufuatia shambulizi hilo
Jumapili, ndege aliyokuwa akisafiria mmojawapo wa maafisa
wakuu wa Sony, ililazimika kubadilisha mkondo kufuatia hofu ya kulipuliwa.
Baadaye ilibainika kuwa kundi linalodai kutekeleza
shambulizi hilo la mtandao, kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter
uliashiria kuwepo kwa tishio la usalama kwa ndege hiyo.
'Kusuluhisha swala hilo
Katika taarifa hiyo Sony ilisema kuwa “mtandao wa
Playstation na mtandao wa burudani wa Sony iliathirika kufuatia jaribio la
kufululizia tovuti zao watumiaji wengi na kuizuia kutoa huduma.
"Tutajitahidi kusuluhisha swala hili na tunatumai kuwa
tutarejesha huduma zetu haraka iwezekanavyo,”
Sony imesema kuwa wapelelezi wa FBI wanachunguza tishio la
usalama kwa ndege aliyokuwa akisafiria rais wa Burudani ya Sony Mtandaoni John
Smedley, ambayo ilitarajiwa kutua San Diego lakini ikalazimika kubadilisha
mkondo na kutua Phoenix, Arizona
Bwana Smedley alituma ujumbe wa tweeter, "Ndio. Ndege
yangu ilibadilisha mkondo. Sitazungumza zaidi ya hayo. Haki itatendeka kwa watu
hawa.”
Mtandao huo wa sony wenye zaidi ya wateja milioni 52 wa Sony
Playstation umewahi kushambuliwa na wavamizi wa mtandaoni hapo awali, likiwemo
shambulizi lililoiba habari za siri za mtandao huo, mwaka 2011.
Baada ya 1740 BST, huduma fulani zikiwemo duka la
PlayStation, akaunti ya usimamizi na usajili ya PSN, huduma za burudani na
michezo ya mtandaoni hazitakuwepo, kwa sababu ya marekebisho.
No comments:
Post a Comment