Raia mmoja wa Venezuela amehukumiwa kwenda jela kwa miezi
mitatu nchini Jamaica baada ya kukutwa na hatia ya kumeza zaidi ya dola laki
moja, fedha taslimu.
Eddy Albeiro Mancipe Ortega alisimamishwa wakati akijaribu
kupanda ndege kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sangster, mjini Montego
Bay kuelekea Trinidad, limeripoti gazeti la Gleaner.
Maafisa walipatwa na wasiwasi wakati wakimhoji Bwana Ortega,
40, na baadaye kumkamata. Alilalamika kuwa anahisi maumivu na kupelekwa
hospitali, ambapo katika siku mbili alizolazwa aliweza kutoa- kupitia njia ya
haja kubwa,- pakiti 80 zilizokuwa na dola 103,500, ambazo alikuwa akijaribu
kutoka nazo kimagendo. Kwa kuwa alikuwa akishikiliwa na polisi kwa miezi minane
kabla ya kushtakiwa na kuhukumiwa wiki hii, amefukuzwa nchini humo mara moja.
Mkuu wa Idara ya upelelezi wa fedha Justin Felice amesema
Jamaica itaimarisha upekuzi katika viwanja vya ndege na katika bandari, na
kuongeza "hili ni tukio la kwanza kuona fedha zikisafirishwa kwa mtindo
huu kutoka Jamaica. Inaonesha jinsi watu wanavyoweza kujaribu kuepuka mkono wa
sheria wenye lengo la kupambana na ulanguzi wa fedha
No comments:
Post a Comment