Wakati wakongwe wao wakitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki leo jijini Dar es Salaam, Real Madrid imeshindwa kuonyesha kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid.
Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou.
Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo katika dakika ya 2 tu.
Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza kupindua matokeo.
Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.
|
No comments:
Post a Comment