WATU watano (5) wamekufa na wengine ambao idadi yao
haijafahamika mara moja kujeruhiwa vibaya, baada ya gari walilokuwa wanasafiria
mali ya Kampuni ya Hood, lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam,
kugongana uso kwa uso na daladala (kifodi) inayofanya safari zake kati ya
Arusha mjini hadi Tengeru katika eneo la Kilala mapema leo asubuhi.
]Mashuhusda wa tukio hilo wameiambia blogu hii leo Agosti 2,
2014 kuwa ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likiwa katika mwendo kasi na
kutaka kulipita lori la mafuta lililokuwa liko mbele yake na kusababisha
kugongana na daladala hiyo na kupelekea watu watano kufa papo hapo.
Taarifa za awali zinasema kuwa, mara baada ya ajali kutokea
dereva wa basi la Hood alijaribu kukimbia lakini wananchi waliweza kumtambua na
kumkamata kutokana na sare alizovaa.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kuwa taarifa zaidi itatolewa baada ya
kujua idadi ya majeruhi na watu waliopoteza maisha kutokana na baadhi ya
majeruhi kuwa na hali mbaya.
Amesema majeruhi wa tukio hilo wamepelekwa katika Hospitali
ya mkoa wa huo Mount Meru.
Blogu hii inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu pindi
tutakapopata taarifa zaidi tutawaletea.




No comments:
Post a Comment