Huku ikiwa ugenini, Arsenal imefanikiwa kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Besiktas ya Uturuki.
Mechi hiyo ya kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ilikuwa ngumu kila upande ukapoteza nafasi nyingi.
Demba Ba pia angeweza kufunga katika nafasi mbili alizopata lakini haikuwa hivyo.
Mwishoni mwa mchezo huo, Arsenal ilipata pigo baada ya Aaron Ramsey kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mechi ya pili mjini London ndiyo itakayotoa majibu, wakati sare yoyote ya mabao itakuwa na faida kwa Besiktas wakati Arsenal licha ya kuwa nyumbani watatakiwa kushinda.
No comments:
Post a Comment