MFUNGAJI bora wa kombe la dunia lililomalizika majira haya
ya kiangazi nchini Brazil, James Rodriguez alifunga bao lake la kwanza Real
Madrid, lakini halikuweza kuipa ushindi timu hiyo ya Carlo Ancelotti dhidi ya
Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Super Cup.Raul Garcia aliisawazishia
Atletico kwa kuunganisha mpira wa kona zikiwa zimesalia dakika tatu tu mpira
kumalizika.
Real wangeweza kushinda baada ya kufanya shambulizi hatari
dakika za mwisho, lakini Mario Suarez aliweza kuzuia shuti lililopigwa na Dani
Dani Carvajal.
Katika mchezo huo, mshambuliaji tegemeo wa klabu hiyo,
Mreno, Cristiano Ronaldo alitolewa nje wakati wa mapumziko na kumpisha
Rodriguez. Madrid.
Ni mimi! Raul Garcia (kushoto) akishangalia baada ya
kuisawazishia Atletico Madrid katika dimba la Bernabeu
James Rodriguez alijiunga na Real Madrid kutokea klabu ya
Monaco majira haya ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 60
No comments:
Post a Comment