TUHUMA nzito ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo
mkazi mmoja wa Tandale – Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini, Idd Mpenda
anadaiwa kumshambulia na kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati
akiswali.Akizungumza na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo alisema
tukio hilo lilijiri Julai 28, mwaka huu saa saba mchana wakati akiswali maeneo
ya duka lake lililopo Tandale.
ILIKUWA KUSHTUKIZA ::Alidai kwamba alikuwa katika
kusujudu, mara mumewe alitokea na
kumshambulia kwa mateke, ngumi na viatu kisha akamburuza chini hadi nje hali
iliyosababisha nguo aliyovaa kuvuka na kubaki kama alivyozaliwa!“Kama
unavyoniona, nimeumia sehemu mbalimbali za mwili. Kiatu ndiyo kimeniumiza sana.
Majeraha ya mguuni aliyopata Bi. Nasra Dafa.
ATINGA KITUO CHA POLISI
Alisema baada ya tukio hilo kutokea alijivuta na kuvaa gauni lingine kisha
akakimbilia Kituo Kidogo cha Polisi Tandale ambapo polisi walimwambia ishu yake
ni nzito na kumtaka aende Kituo cha Polisi Magomeni (vyote vipo Dar).
ASIMULIA VIPIGO, UKE WENZA
Mwanamke huyo aliweka hadharani kwamba mumewe amekuwa
akimpiga mara kwa mara na tatizo kubwa ni uke wenza ambapo alidai ameoa mke wa
pili hivi karibuni na mapenzi baina yao yamezorota.
“Mimi kabla ya kufunga naye ndoa Januari Mosi, 2013 mume
wangu alikuwa na mke mwingine lakini aliamua kumpa talaka baada ya kumweleza
kuwa mimi sitaki kuwa mke mwenza.
“Tukawa tunaishi naye lakini hata hivyo hakuchukua muda
mgogoro ukaanza ndani ya nyumba.
Picha hii ikionyesha majeraha ya mkononi na shingoni
aliyopata Bi. Nasra Dafa.
SAKATA LAFIKA KWA NDUGU
Mwanamke huyo aliendelea kusema kwamba hali ilizidi kuwa
mbaya hadi ikafika kwa wana ndugu kwa suluhu, walipatanishwa lakini baada ya
muda mgogoro ukaendelea na kuna siku mumewe akamwambia ameoa mke mwingine wiki
tatu nyuma.
SIKU YA TUKIO
“Siku ya tukio, nilikuwa naswali. Unajua wakati wa Mfungo wa
Ramadhani lazima Muislam kuswali kwa kuzingatia taratibu zote za dini. Basi,
alikuja na kuniita nitoke nje lakini sikutoka.“Niliona nimalize kwanza
kuswali ndipo nitoke, lakini kabla
sijamaliza akaja na kunishambulia kama niliovyokwambia kisha akachukua funguo
na kufunga duka.
Amani lilifika kwenye Kituo cha Polisi Magomeni na kuambiwa
na askari mmoja kuwa taarifa hizo zipo na mtuhumiwa anashikiliwa hapo, lakini
akashauri atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura
kwa maelezo zaidi. Kamanda huyo hakupatikana ofisini kwake hadi tunakwenda
mtamboni.
SHEHE MKUU ASAKWA
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum
hakupatikana kuzungumzia makosa ya mume wa Kiislamu kumpiga mkewe wakati
akiswali ndani ya Mwezi Mtukufu.Hata hivyo,
Maalim Hassan Yahya Hussein wa Magomeni Mwembechai alipoulizwa
alisema Uislamu haujatoa ruhusa kwa
mwanaume kumpiga mkewe wakati anaswali hata kama amefanya kosa kubwa kiasi
gani.
“Uislamu haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji na kuna
hadithi zinazokataza mtu kumdhuru mwenzake. Kuna masharti sita yamewekwa kabla
ya mume kufikia hatua ya kumwadabisha mkewe,” alisema Maalim Hassan.Akaendelea:
“Kabla mume hajampa adhabu mke anapaswa kwanza kumpa nasaha kwa kosa alilotenda
na sharti la pili ni kumpa mawaidha ama yeye mwenyewe au atafute mtu.
“Sharti la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara na sharti la nne ni kumhama malazi, yaani
kumuacha alale peke yake. Sharti la tano, akikosa ni kwenda kushitaki kwa wazee
au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa kadhi na viongozi wa dini.“Sita ndiyo
kumpiga, lakini kipigo ambacho hakitamdhuru kwani hutakiwi kumpiga ukiwa na
hasira.”
No comments:
Post a Comment