Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamsaka Mwenyekiti wa
serikali ya kitongoji kimoja katika kata ya Kahe, wilaya ya Moshi kwa tiketi ya
CCM, ambaye ametokomea kusikojulikana baada ya wananchi kufichua shamba la bangi
lenye ukubwa wa robo ekari analomiliki.
Mbali ya shamba hilo kugunduliwa, nyumbani kwa kiongozi huyo
polisi pia walikamata kilo 30 za bangi, ambazo zilikuwa mbioni kusafirishwa
kwenda kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, jana
alisema makachero wa jeshi hilo wanamtafuta kwa udi na uvumba mwenyekiti huyo,
ambaye amekimbia baada ya kubaini anatafutwa kwa kosa la kulima bangi na
kuhifadhi dawa hizo za kulevya nyumbani kwake kinyume cha sheria za nchi.
“Bado tunamtafuta huyu mwenyekiti lakini pia katika msako
ulioendelea siku hiyo pia tulimbaini mkulima mwingine ambaye ana shamba la
bangi robo ekari katika kijiji cha Kisange Sangeni, kata ya Kahe. Hawa wote
wawili wamepanda na kustawisha bangi katikati ya shamba la mahindi


No comments:
Post a Comment