Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
-------------------------------
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
Pamoja na kuwepo kwa harakati na utetezi kuhusiana na haki za
watoto ikiwemo ya kuishi lakini bado wilayani Songea mkoani Ruvuma kumeendelea
kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoambatana na utupaji wa
watoto wachanga.
Vitendo hivyo ni pamoja na kitendo kilichotokea jana katika
mtaa wa Lizaboni mjini Songea ambapo mwili wa mtoto mchanga anaedaiwa kuwa na
umri wa miezi sita ulikutwa ukiwa umefukiwa ndani ya nyumba moja ambayo
haikaliwi na mtu katika eneo hilo inayomilikiwa na Olaph Ngalika.
Akizungumzia tukio
hilo balozi wa mtaa huo Juma Kanganya amesema taarifa za kuwepo kwa mwili huo
zilitolewa na mafundi waliokuwa wakijenga nyumba hiyo ambaye alisema wanahisi
kuwepo kwa kiumbe kilichofukiwa ndani ya nyumba hiyo ambacho kinafanana na
binadamu.
Amesema baada ya
kupata taarifa hiyo walitoa taarifa polisi ambao walifika na kufukuwa na kukuta
sehemu ya mwili wa kichanga kinachodaiwa kuwa na umri wa miezi sita kitendo
ambacho mbali ya kuwasghangaza mashuhuda wa tukio hilo lakini wamelionba jeshi
la polisi mkoani Ruvuma kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kuwabaini wahusika
wa tukio hilo la kikatili.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi
ili kubaini wahusika wa kitendo hicho ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
dhidi yao huku baadhi ya wanaharakati wa haki za watoto wakitoa wito kwa jamii
mkoani Ruvuma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuweza kudhibiti
vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment