Mtoto Zahara Almeda aliyegongwa na polisi huyo.
MOROGORO. Polisi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara
moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga
mtoto wa kike, Zahara Almeda katika barabara ya Mji Mpya.
Katika tukio ambalo mwandishi wa habari hizi
alilishuhudia,
mara tu baada ya kumgonga mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua magimbi na
mihogo, askari huyo aliteremka na kukimbia akiliacha nyuma gari lake lililokuwa
bado halijazimwa, ambalo ndani yake kulikuwa na kofia yake.
Polisi wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio.
Wananchi waliojawa na
hasira baada ya tukio hilo walilizingira gari hilo na kutaka kulichoma moto,
lakini busara za baadhi yao ziliwezesha kitendo hicho kutofanyika na baadaye
trafiki alifika kudili na tatizo hilo.
Mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo iliyolihusu gari aina
ya Toyota Baloon lenye namba za usajili T 5** AUE, alisema mtoto aliyegongwa
alikuwa akitokea sokoni Mji Mpya, akiwa amebeba kikapu kichwani. Mtu huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kiwamba, alisema binti huyo alikuwa
ameshavuka barabara, lakini wakati akijiandaa kuvuka msingi wa pembeni gari
hilo lilimfuata katika jitihada za kumkwepa mwendesha pikipiki.
Watu wakishuhudia tukio hilo.
Hata hivyo, siku moja
baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo
alisema mwanaye anaendelea vizuri na mtu aliyemgonga alikwenda hospitalini
kumjulia hali kwani aliamini alikuwa amefariki.
No comments:
Post a Comment