Umoja
wa Mataifa umeonya kwamba maambukizi ya Ebola huenda yakaongezeka na kutimia
20,000 kufikia mwezi Novemba iwapo juhudi za kudhibiti ugonjwa huo
hazitaongezwa maradufu.
Marekani
imeonya kwamba huenda maambukizi mabaya zaidi yakashuhudiwa Januari mwakani
ambapo maambukizi katika ukanda wa Afrika Magharibi huenda yakagonga milioni
1.4.
Hata
hivyo wadadisi wamesema makadirio hayo ya Marekani hayapendezi wala hayaonyeshi
nia nzuri.
Mlipuko
huo wa ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo 2,800, visa vingi vikiripotiwa katika
mataifa ya Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Shirika
la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema mkurupuko wa ugonjwa huo ‘‘ulidhibitiwa
vyema” nchini Nigeria na Senegal.
Wanasayansi
wamesema hatua madhubuti zinafaa kuchukuliwa ili kuzuia kuenea zaidi kwa
maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.
Inakadiriwa
kwamba maambukizi ya Ebola huenda yakaongezeka zaidi katika mataifa matatu
yalioyoathirika zaidi.
Uchambuzi wa visa vilivyoripotiwa tayari unaonyesha kwamba
idadi ya watu wanaofariki imeongezeka mpaka 70% kutoka asilimia 50%.
Afisa wa WHO, Bw. Christopher Dye ameonya kwamba ikiwa hatua
za
haraka za kudhibiti ugonjwa huo hazitachukuliwa, maelfu ya visa hivi
vitazidi kuripotiwa kila juma katika mataifa hayo matatu.
Wakati huo huo wakfu wa Wellcome uimetangaza kwamba dawa za
kuponya ugonjwa huo zitafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza huko Afrika
Magharibi.
Moja ya dawa hizi inafahamika kama ZMapp ambayo tayari
imepatiwa baadhi ya wagonjwa wa Ebola.
Dkt Peter Horby, kutoka Centre for Tropical Medicine and
Global Health iliyo katika chuo kikuu cha Oxford, amesema majaribio rasmi ya
dawa hizo yataanza Novemba, Afrika Magharibi.



No comments:
Post a Comment