Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye tajiri mkubwa zaidi
nchini Uchina kulingana na rekodi za kampuni yake.
Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha ya Hurun.
Bw.Ma ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi nchini Uchina
kwa mali ya takriban dola bilioni 25 akifuatwa na mwenyekiti wa Wanda Group
Wang Jianlin.
Matajiri watano katika ya kumi walio katika orodha
hiyo,
wanamiliki kampuni za mitandaoni huku wakiwabwaga wale wanaomiliki mali
isiyohamishika ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiongoza orodha hiyo.
Matajiri nchini Uchina
JINA KAMPUNI
(Thamani Dola za Marekani US$)
1. Jack Ma Yun Alibaba (Teknohama) $25bn
2. Wang Jianlin Wanda ( Uwekezaji, burudani) $24.2bn
3. Li Hejun Hanergy (kawi) $20.8bn
4. Zong Qinghou Wahaha (Vinywaji) $20.8bn
5. Pony Ma Tencent (Teknohama, burudani) $18.1bn
Orodha hiyo inahusisha pia kiongozi wa Tencent Pony Ma.
Mabwenyenye wengine walio katika orodha hiyo ni mwanzilishi
mwenza wa mtandao wa intanet marufu sana nchini China Baidu, Robin Li na pia
mwanzilishi wa soko la mtandao la JD.com, Richard Liu Qiangdong.


No comments:
Post a Comment