Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan, amekanusha
madai kuwa alimtoa kafara yake ambaye pia alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini
Ghana Castro.
Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina
msingi.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa
Afrobeats, ambaye jina lake halisi ni
Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na
rafiki yake Janet Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na
Gyan ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.
Madai katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa
kutoweka kwa rafiki ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa
kafara mwanamuziki huyo.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho
wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.
Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai
yaliendelea kusambazwa mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan
alidaiwa kuwa mmoja wa genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari
waliohoji maswali kuhusu madai hayo.
Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata
kwa lengo la kumfungulia mashitaka.
Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa
habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa
familia ya Gyan imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote
ili polisi waendelee na uchunguzi wao.
Taarifa hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya huku madai na
tetesi zikienezwa kila upande katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti
kwa sababu tunaficha ukweli, bali kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema
kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa sababu tunataka polisi wafanye kazi
yao bila kuingiliwa.''


No comments:
Post a Comment