Jeshi nchini Nigeria limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko
Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo limesema katika mapambano limemuua mtu mmoja
ambaye huwa anaonekana kwenye picha za video za propaganda za Boko haram
akijidai kuwa Kiongozi wa wa kundi hilo, Abubakar Shekau.
Jeshi lilisema kuwa wapiganaji 135 walijisalimisha wakiwa na
silaha zao katika eneo la Biu , jimbo la
Borno siku ya Jumanne. Liliongeza kuwa
wengine 133 walijisalimisha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Lagos Will Ross anasema
kuwa ni vigumu kuthibitisha madai hayo ya jeshi.
Mwaka jana jeshi lilisema kuwa Shekau huenda aliuawa ,
lakini halikutoa thibitisho lolote.
Hata hivyo ikiwa ni kweli kuwa wapiganaji hao wamejisalisha
basi huenda ni ushindi kwa jeshi la Nigeria katika vita vyake dhidi ya Boko
Haram.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa majuma ya hivi
karibuni Boko Haram imeshindwa kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa wakipambana
kudhibiti eneo karibu na mji wa Maiduguri ambalo ni ngome yake.
Jeshi limesema wafuasi 135 wa Boko Haram wamejisalimisha
wakiwa na silaha zao katika majimbo ya Biu na Borno,halikadhalika wafuasi
wengine 133 wanahojiwa.
Kwingineko , Rais wa Nigeria,Goodluck Jonathan amesema kuwa
zaidi ya watu 13,000 waliuawa katika miaka mitano ya kwanza ya harakati za Boko
Haram nchini humo.
Rais Jonathan alisema hayo katika hotuba yake katika baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumatano.
Rais Jonathan pia alisisitiza kuwa juhudi zinafanywa
kuwaokoa wasichana wa Chibok.chanzo Bbc


No comments:
Post a Comment