Na Sensei Rumadha Fundi
KUTAFAKARI/MEDITATION
Kutafakari "Meditation" au katika lugha ya Sanskrit "Dhyana" ama mtiririko wa mawazo ni moja ya sehemu kuu Yoga inasisitiza
kuidumisha katika sanaa hii ya upanuzi wa mawazo.
Falsafa ya Yoga inaamini kwamba ubongo wa mwanaadamu
unatoa msisimko wa mawimbi ambayo huwasumbua sana binaadamu kuweza kutumia
uwezo wao wa fikra katika asilimia 100, na hatimae
mwanadamu hutumia tu asilimia 1, ya fikra zake na zote asilimia 99 hupotea kutokana na upungufu wa utulivu wa mawazo ya mwanaadamu ( Concentration/ Focus).
mwanadamu hutumia tu asilimia 1, ya fikra zake na zote asilimia 99 hupotea kutokana na upungufu wa utulivu wa mawazo ya mwanaadamu ( Concentration/ Focus).
Hivi karibuni tu, uvumbuzi mpya wa sayansi
ya Yoga amegundua kwamba ubongo wa mwanaadam umejengwa katika mchanganyiko wa
mabillion ya "Nervr Cells, hatimae kutoa mkondo mdogo wa umeme ( tiny electric current) ijulikanayo kama "Brain waves" ambayo hubadilika kila sekunde kufatana na mabadiliko
ya nguvu za ufahamu wako katika ubongo. Mashine yenye uwezo wa kuweza soma
mawimbi hayo ya ubongo hujulikana kama "EEG", au "Electroencephalogram" Chombo hiki kinapo fungwa kichwani
mwa binaadamu hutowa mawimbi na kuyasajiri kupitia mashine ya computer screen
na kutoa mawimbi yenye kina tofauti kutokana na nguvu za ubongo wa mtu.,
yaitwayo:
Beta Wave:
span lang="EN-US" style="font-family: "Cambria","serif"; font-size: 12.0pt; mso-ascii-theme-font: major-latin; mso-bidi-font-family: Aharoni; mso-hansi-theme-font: major-latin;"> Mawimbi ya mizunguko 13 kwa dakika ya ubongo :
kutokuwa na utulizu wa fikra'Stress/
Restless"
Alpha Wave:
Mawimbi
ya mizunguko 8 kwa dakika: msukumo imara kidogo wa nguvu "Steady and rythmic Amplitude".
Theta Wave:
Mawimbi
ya 4 kwa dakika: Mawazo yenye
nguvu za ubongo, ubunifu na usanifu wa kisayansi ubongo umetulia.
Delta Wave:
Wimbi la 1 kwa dakika.
Hapa nikupitia tu njia ya kutafakari ndio mtu huweza kufikia hatua hii ya wimbi
moja kwa dakika. Ubongo wenye nguvu zisizo kawaida " Intuitive mind/ subtler mind". Moja ya ngazi hii ina uwezo wa kuwa utabiri
wa matokea ya mbele kutokana na upeo wa
fikra.
Lengo kuu la "Meditation" ni kuwa na uthibiti wa
mawimbi ya ubongo kuweza kupunguza kasi yake toke a mawimbi 13 kwa sekunde
hadi wimbi 1 kwadakika na ubongo huo ndio upo katika
watu wenye upeo wa fikra zilizotulia kama maji ndani ya mtungi. Maji ya mtungi
au kisima yakitulia ina kuwa kama vile kioo, ukiangalia ujiona mwenyewe. Kama
maji yakitibuliwa hutoawa mawimbi mengi na kusababisha mvurugano nakutoweza
kuona kimvuli chako mwenyewe au " Reflection."
Kupitia sauti itwayo "Matra", ubongo hutumia mbinu hiyo
kama chombo cha kukufikisha pale unakotaka kwenda. Pia Yoga ina masomo ya ngazi
nyingi (Lessons).
Moja ya vitu sanaa Yoga inasaidia kuweza
kumudu (Control) ya hisia zako
mwilini yaani " Emotion", "propensities" kusaidia " Secretions of Hormones" kumudu hasira kupitia mazoezi yenye
utafiti wa kuiga mikao ya wanyama
kadhaa na ndege ambayo inaaminika wanatumia kwa kujitibu
wenyewe. bila kutumia dawa. Mikao yote ya Yoga (Yoga Postures) inasaidia matatizo kama vile:
Shindikizo la damu( High blood Pressure), uzito wa mwili ( Obesity), kisukari ( Diabetes) na matatizo kadhaa ya magonjwa
ya wanawake. Hivyo basi, Yoga ina faida nyingi mno ambazo watu wengi
hawazifahamu.
Yoga inaamini kwamba, kuna sehemu 7
za nguvu ndani ya mwili wa mwanaadamu
kupitia uti wa mgongo au "Kun'da'alini " katika lugha
ya Sansrit ( Coiled Serpentine).
Sehemu hizo ni :
1.Muladhara
Chakra: ipo katika mkia wa ya uti wa
mgongo
2. Sva'dhis;tha'na Chakra:ipo
sehemu ya kizazi (Groin area)
3. Man'ipu'ra
Chakra: ipo kitovuni.
4. Ana'hata
Chakra katika ya kifua.
5. Vishuddha
Chakra: ipo koromeo (Thyroid Gland)
6. A'jna
Chakra: ipo katikati ya macho (Pituitary).
7. Sahasra'ra Chakra: Ipo katika utosi.
Mwafunzi anapozidi kuendelea kwa kina
katika sanaa ya Yoga, ndipo anapo pita hizo sehemu ya nguvu 7 katika uti wa mgongo
na hatimaye kufikia hatua ya kuwa na udhibiti wa hizo hisia zake mwenyewe
au "Propensities".
Sayansi ya Yoga nipana sana yenye
kina kirefu na filosofia yenye karne. Mazoezi ya Yoga husaidia viungo vya ndani
ya mwili (Internal Organs) kama vile
moyo,figo, maini, kwa kuvikanda ( massage)
zaidi ya mwili wanje. Tofauti ya mazoezi ya gym na Yoga ki kwamba: Ukifanya
mazoezi gym ( vigorous exercise) unatumia sana nguvu na kuchoka haraka, wakati
mazoezi ya Yoga ( Yoga Asanas)
unalinda nguvu za mwili (Conserve Energy)
hata kama na umri wa uzee sana na kuwa umetulia (Relax). Yoga ina njia yake ya tiba vilevile ijulikanayo kama: "Yogic treatment and remedies"
Haya ni machache tu kuhusu nini hasa
faida ya mazoezi ya yoga na mazoezi aina nyingineyo.
Sensei Rumadha pia ni mkufunzi wa
sanaa ya Karate mtindo wa "Okinawa Goju Ryu Jundokan Kyokai". Kabla ya hapo, hususan akiwa nyumbani Tanzania, Sensei Rumadha alikuwa mmoja wa wanafunzi waandamizi wa Marehemu Sensei Nantambu Camara Bomani ambaye ni mwanzilishi wa mafunzo ya karate aina ya Goju Ryu pale Zanaki, jijini Dar es salaam miaka ya 1980.
No comments:
Post a Comment