Rapper wa kike Witness amepata bahati mbaya baada ya
ujauzito wake wa miezi nane na nusu kuharibika.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Witness ameeleza kuwa
alikuwa anatarajia mapacha na alikuwa katika hatua za mwisho lakini ghafla
ikatokea hali hiyo ambayo hadi sasa inafanyiwa uchunguzi na madaktari kubaini
chanzo.
“Kuna mambo ambayo niliambiwa kwamba endapo ningekuwa sina
mazoezi au ningekuwa siko strong ina maanisha kwamba na mimi mwenyewe ningekuwa
hatarini.” Amesema Witness.
Ameeleza kuwa hali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita lakini
yeye na mchumba wake Ochu waliamua kukaa kimya kwa muda hadi leo walipoamua
kuiweka wazi.
Akiongelea afya yake, member huyo wa zamani wa WAKILISHA
ameeleza kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.
Tunampa pole kwa tatizo hilo lililomkuta na tunamuombea awe
na afya njema kama zamani.


No comments:
Post a Comment