UMOJA wa Katiba ya Wananchi “Ukawa” wamemtaka Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, kuzuia mikutano ya Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana,
kama alivyozuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa vinavyoundwa
na Ukawa.
Hayo yamezungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lissu
wakati akizungunmza na waandishi wa habari leo, makao makuu ya chama hicho,
Kinondoni jijini Dar es Salaam .
Aidha umoja huo umetoa tamko juu ya amri ya Mahakama Kuu ya
Tanzania kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba kwa kumuunga mkono Saed
Kubenea aliyekuwa amefungua kesi ya
kuitaka
Mahakama Kuu itoe ufafanuzi wa mamlaka ya bunge hilo kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha sheria ya
mabadiliko ya katiba, sura ya 83 ya sheria za nchi yetu.
(Habari/Picha na:
Gabriel Ng’osha/GPL)

No comments:
Post a Comment