Mwalimu wa kanisa Katoliki, Magharibi ya Kenya alijikuta
taabani baada ya kutekwa nyara na majambazi waliomtesa pamoja na kumpiga
msumari kwenye mti msituni, umbali wa kilomita miambili kutoka nyumbani kwake.
Peter Asutsa alikaa msituni kwa saa 16 mkono wake
ukiwa
unaning'inia kwenye mti kabla ya kuokolewa na polisi.
Inaarifiwa Peter alipigwa msumari kwenye kwenye mkono wake
mmoja baada ya majambazi hao kukosa kumpata na pesa zaidi walizokuwa wakitaka.
Inaarifiwa Asutsa aliizima simu yake na kuificha ndani ya
nguo zake za ndani ambapo majambazi hao wasingeweza kuipata.
Baada ya majambazi hao kumtelekeza, alimpigia simu mkewe
ambaye aliwaarifu polisi waliokuja kumuokoa.
Masaibu ya Asutsa yalianza pale alipokwenda dukani
kumnunulia mkewe mgonjwa dawa katika duka la dawa mjini Kitale Magharibi ya
Kenya.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari alimokuwa anasafiria
Asutsa aliamrisha dereva kusimamisha gari. Kisha akawafungia ndani akiwa na
abiria wengine wawili.
Alitekwa nyara na majambazi waliofika katika sehemu hiyo kwa
gari jingine na kumuingiza ndani ya gari hilo na hapo ndipo alipogundua kuwa
alikuwa ametekwa nyara.
Walimpora dola 24 na kumtaka asalimu simu yake , lakini
akataa.
Baadaye walimpeleka ndani ya msitu na kumpigia msumari mtini
kupitia kwenye mkono wake mmoja na kumuacha ndani ya msitu wa Kaptagat.
Alilazimika kuwatisha na kuwafukuza Fisi na Mbweha waliokuwa
wakitishia kumvamia usiku.
Aliambia BBC kuwa alihisi maumivu makali.
No comments:
Post a Comment