Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 3, 2014

MCHINA IRINGA ACHEZEA KICHAPO KWA KULAZIMISHA PENZI KWA MKE WA MTU,TUKIO LIKO HAPA


 Mchina  akichezea  kichapo kwa kumshika mke wa mtu maziwa mjini Iringa 

...................................................................................................


RAIA  mmoja  wa Kichina ambae  jina lake  halikuweza  kupatikana mara  moja anayesadikika kuwa ni mmoja kati ya mafundi katika ghorofa  moja  mjini Iringa amejikuta akichezea  kichapo kutoka kwa  njemba mmoja ambae  alikuwa ameongozana na mke  wake  baada ya mchina  huyo kumshika maziwa mwanamke  huyo akimtaka mapenzi  mbele ya mumewe .





Tukio  hilo  lililofananishwa na udhalilishaji kwa  wanawake  lilitokea jana majira ya saa 2 usiku katika  eneo la stendi ya  daladala  za Mkwawa  kata ya Miyomboni mjini Iringa.







Kutokana na  kitendo hicho  cha aibu alichokifanya mchina  huyo mume wa mwanamke huyo alikosa  uvumilivu na bila  kujali kuwa  wachina ni wataalam  wa kareti alimvaa mchina  huyo na kumpiga mtama uliopelekea  kuanguka  chini  na  kuwafanya  vijana  wapiga debe eneo hilo kuanza  kumshambulia kwa kichapo  bora  mradi   wamepigana na mchina .




Vijana  wakimpa kichapo mchina  huyo 
Mashuhuda wa  tukio  hilo  waliueleza mtandao huu wa matukiodaima.co.tz  uliofika kwa wakati  eneo la  tukio  kuwa mchina  huyo alikuwa akitoka katika eneo la jengo  wanalolijenga  lililopo jirani na stendi hiyo na baaada ya kufika eneo hilo la Stendi alikuta  watu  wengi  wakiwa  wanasubiri usafiri wa daladala kwenda  Mkwawa na Ilala na bila   aibu mchina  huyo alimsogelea mwanamke  huyo ambae  pembeni alikuwa na mume  wake na kumshika maziwa  yake  mfano  wa kumtaka penzi kwa  nguvu jambo ambalo  lilimfanya mwanamke  huyo  kupiga  kelele  huku mchina  huyo akimsemesha  kichina ambacho hakuna  aliyejua anazungumza  nini zaidi ya  kutambua  ishara za  mikono ambazo mchina  huyo alikuwa akionyesha  kuashiria kumwita .


Hapa  akionyesha  eneo lake la kazi 

.........................................................................





Kichapo  kikali alichokipata  mchina  huyo ambae  muda  wote  alikuwa akilalamika kwa  kilio  cha  kichina  ilimfanya mmoja kati ya askari anayeendesha  biashara  zake eneo hilo anayetambulika kwa jina moja la Rashid  kufika  kunusuru ugomvi  huyo na baada ya kutamkiwa  Polisi mchina  huyo alipiga magoti na kuonyesha  ishara za kutubu kosa na askari  huyo alisikika akisema umefanya kosa  huwezi mshika mwanamke maziwa hadharani na  kuachiwa .


Hata  hivyo imedaiwa  kuwa ni  tabia ya mchina  huyo na  wenzake wanaofanya kazi katika jengo  hilo kunyanyasa wanawake na kuwavunjia heshima  zao mbele ya  hadhara  kiasi cha baasi na maeneo ya  pombe vidanda vya UVCCM kiasi cha  kupigwa marufuku kuingia katika baadhi ya vibanda

No comments:

Post a Comment