PIX 1.
Sheikh Hemed Jalala akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (hayupo pichani) wakati alipotembelea Bunge Maalum  03 Septemba, 2014 kwa ajili ya kumpongeza kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya.

 
Na Magreth Kinabo, Dodoma.
BAADHI ya viongozi wa dini wamempongeza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kwa kitendo chake cha kuliendesha Bunge  hilo vizuri katika hali ya utulivu na amani.
Kauli hiyo imetolewa leo na  Sheikh Hemed Jalala kutoka Msikiti wa Ghadiir uliopo maeneo ya Kigogo Post jijini Dares Salaam, ambaye aliambatana na Masheikh wengine ambao ni  Alhaji Mohamed Mputa, Sheikh Mohamed Abdi na Masoud Mbilili.
Aidha  Sheikh Jalala akizungumza kwaniaba ya viongozi wenzake wa dini alisema kuwa wamekuja kutembelea Bungeni hapo kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Sitta na kumuunga mkono kwa kazi nzito nzuri anayoifanya huku akisisitiza kuwa wako nyuma yake katika suala hilo.

“Pamoja na changamoto zilizojitokeza umeweza kukabiliananazo vizuri. Sisi na wananchi kila tunapolifuatilia tunaona mmeweza kulipeleka vizuri. Jambo hili ni zito linahitaji amani, utulivu na kuvumiliana,” alisema Sheikh Jalala.
PIX 2.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akimsikiliza Sheikh Hemed Jalala (hayupo pichani) wakati alipotembelewa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.
Sheikh Jalala alisema wao kama viongozi wa dini, wameona kuna changamoto ya maadili hivyo, wameandaa kitabu maalum kinachoitwa ‘Kilele cha Fasaha’.
Alisema kitabu hicho kitasaidia kutoa mchango wao kwenye masuala ya uongozi na maadili, ambacho alikikabidhi kwa Mhe. Sitta.
Akipokea kitabu hicho, Mhe.Sitta amesema ni jambo la baraka kwake, ambapo aliahidi kutoa taarifa juu ya jambo hilo na kukikabidhi kitabu hiko katika Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo.
PIX 3.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusiana na maendeleo ya Bunge hilo wakati alipotembelewa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo na kushoto ni Sheikh Hemed Jalala.
Sheikh Jalala alisema kuna jumla ya nakala 632 ya vitabu hivyo na vimeshakabidhiwa kwenye ofisi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo.
Katika hatua nyingine Sheikh Jalala ameongoza dua maalum kwa ajili ya kuliombea Bunge hilo ili liweze kuendelea kwa amani, utulivu, busara, maelewano na upendo.
PIX 4.
Baadhi ya viongozi wa Dini waliofuatana na Sheikh Hemed Jalala wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (hayupo pichani). Wa kwanza kulia ni Alhaj Mohamed Mputa na anayemfutia ni Sheikh Mohamed Abdi.
PIX 5.
Baadhi ya Waandishi wakifuatilia mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na mgeni wake Sheikh Hemed Jalala  03 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PIX 6.
PIX 7.
Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wa kwanza kulia)  03 Septemba, 2014 mjini Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo.
PIX 8.
Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akikabidhi kitabu kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (kulia),  kinachoitwa ‘Kilele cha Fasaha’ kinachohusu maadili na uongozi.
 PIX 9.
Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akiongoza dua ya kuiombea Bunge Maalum la Katiba. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta na katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo.
PIX 10.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Sheikh Hemed Jalala (kulia) mara baada ya kukamilisha mazungumzo yaliyofuatana na dua maalum ya kuiombea Bunge hilo leo 03 Septemba, 2014.
PIX 11.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Hemed Jalala (wa pili toka kushoto) pamoja ujumbe aliofautana nao. Wa kwanza kulia ni Alhaj Mohamed Mputa, anayemfuatia ni Sheikh Mohamed Abdi na wa tatu toka kulia ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo.(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).