Kanisa lililoporomoka mjini Lagos wiki jana , na kuwaua watu
wengi, lilikuwa linamilikiwa na mhubiri anayesifika sana nchini Nigeria, TB
Joshua.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anatufichulia haiba ya mhubiri
huyu ambaye anadai amewaponya watu wakiwemo vipofu na waathiriwa wa HIV.
TB Joshua anadai kuwahi kutabiri matukio mengi kuanzia kwa
kifo cha aliyekuwa gwiji wa muziki, Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya
Malaysia ya MH370"
Anajiita mtume na ni mmoja wa wahubiri mashuhuri sana nchini
Nigeria ambako makanisa kama lake ni mengi kupindukia.
Alizaliwa mwaka 1963 tarehe 12 Juni katika familia maskini,
akidai kwamba alikaa kwenye tumbo la mamake kwa miezi 15.
Baadaye katika maisha yake, anadai kuona kwenye ndoto yake
manabii wakimtaka kuhubiri na
kufanya miujiza.
Hapo ndipo alipoanzisha kanisa lake analoiita, 'Church of
All Nations (SCOAN),' mwanzoni likiwa na waumini 8.
'Maji ya kuponya'
Wanaume na wanawake waanguka sakafuni wakati wakiombewa na
TP Joshua
Hii leo Jushua kama wahubiri wengine nchini Nigeria, ni
tajiri wa kupindukia akishabikiwa sana na watu nchini humo.
Watu huja kwake kutoka kote duniani wakitaka kuombewa
wapone.
Wakati ugonjwa wa Ebola uliporipotiwa katika kanda ya Afrika
Magharibi, serikali ya jimbo la Lagos, ilimtambua muhubiri huyo kwa kuambia
wagonjwa wa Ebola kwenda kwake akawaponye.
Alikubali kuahirisha baadhi ya programu za kanisa lake za
kuponya lakini inaarifiwa alituma chupa 4,000 za maji ya ''uponyo' nchini
Sierra Leone anayosema kuwa yanatibu magonjwa mengi tu.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment