Nay wa Mitego amesema baada ya kukamilisha ujenzi wa studio
yake mpya iitwayo ‘Free Nation Production’ ameamua kumkabidhi producer wake Mr
T Touch kama zawadi kutokana na kazi ambayo amekuwa akimfanyia katika muziki
wake. Akizungumza na Bongo5 jana, Nay amesema kuwa ameamua kufanya hivyo baada
ya kuona kuwa muziki unazaolishwa na producer huyo unamwingizia
pesa nyingi
kuliko malipo anayompa.
“Wasanii tuna maproducer ,maproducer wetu tunajuaga kama
wamekuwa hawaingizi kipato kikubwa sana tofauti na sisi wasanii,’ amesema Nay.
“Producer akikugongea ngoma moja ukimlipa laki tatu wewe
unaweza ukaingiza zaidi hata ya milioni hamsini. Kwa producer aliyekufanyia
hiyo ngoma inakuwa haimtoshi, for reel kabisa naongea kwa mara ya kwanza kwamba
studio yangu imekamilika ambayo nampa zawadi producer wangu ambaye nilianza
naye tangu… nasema nao mpaka leo hii ngoma yangu ya mwisho ya Mr Nay, zote hapa
katikati amefanya yeye. Tumepata tuzo mara mbili, ni vitu ambavyo amefanya
yeye, nimeingiza pesa nyingi lakini hela ambayo nilikuwa namlipa ni ileile laki
mbili, laki tatu haimtoshi! Mimi nimeshaingiza zaidi ya milioni mia moja, mia
mbili.”
“Kwahiyo nilichofanya nimekamilisha studio na nimemkabidhi
kama zawadi yake. Studio inaitwa Free Nation Production. Mimi mwenyewe nitakuwa
nafanyia kazi zaidi kwa sababu nahisi nitakuwa huru zaidi, japo kuwa sio lazima
nifanyie hapo lakini hii ni kama zawadi kwa producer wangu, pia watu wengine
wakihitaji kurekodi watarekodi.”
Bongo5
No comments:
Post a Comment