Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa
katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
|
Tukio hilo limetokea
September 16/ 2014 majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya
Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasio fahamika walitupa
kitu kinacho sadikiwa kuwa ni Bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa
kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatu
waliokuwa doria.
Askari hao waliojeruhiwa ni
WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye unyayo na pajani ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa
kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika
mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel
Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari
hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma
linaendelea na uchunguzi wa kina ili
kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU
amesikitishwa na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusdi na
amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha
wanawasaka na kuwakamata.
No comments:
Post a Comment