Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 12, 2014

Promota wa Diamond mbaroni

HILO
Na Mwandishi wetu
POLISI nchini Ujerumani wamefanikiwa kumkamata Promota mwenye asili ya nchi ya Nigeria ambaye  ndiye  aliyesababisha fujo katika onyesho la  msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ zilizotokea  Agosti  30 mwaka huu  kwenye ukumbi wa Stuttgart nchini Ujerumani .
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Ujerumani  kilisema  kwamba  Jeshi la Polisi nchini humo kilisema hadi kieleweke kwani watamchukulia hatua kali ili iwe fundisho  kwa mapromota  kama huyo.


 Jumamosi iliyopita Awin Williams Akpomie (pichani) alisababisha fujo na kuvunjwa kwa viti , vyombo vya muziki na vitu mbalimbali baada ya mashabiki  kushikwa na hasira  kwa kukosa  burudani ya shoo ya Diamond  ambapo alicheleweshwa na Promota huyo aliyewatangazia  shoo kuanza kufanyika saa nne usiku na badala yake kutaka shoo ifanyike saa kumi alfajiri.


Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Akpomie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya African Party na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara kiasi cha Euro 300,000 sawa na sh. Mil.600  za Kitanzania ambazo anatakiwa azilipe.
Aidha imeelezwa kwamba Akpomie hakuwa na bima ya kulinda onyesho hilo na ukumbi  lilipotarajiwa kufanyika  onyesho hilo ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.
Taarifa za kipolisi zinasema kwamba suala hilo  tayari zimepeleka  suala hilo  kwa ofisi ya Sheria ya mji wa Stuttgart zilikotokea fujo hizo  ili  sheria ichukue mkondo wake.Hadi sasa bado Polisi wanaendelea kumhoji  Akpomie kutokana na tetesi kwamba najihusisha na biashara zingine za haramu.
Wakati huo huo Taasisi mbali mbali na jumuiya za Wafrika nchini Ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa Nigeria Akpomiemie  kwa  kuwadanganya mashabiki  na kulivunjia hadhi sifa za bara la Afrika nchini  humo  , pia taasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa .

No comments:

Post a Comment