Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 29, 2014

SHERIA YA BUNGE YAZUA KILIO KWA VIZIWI ARUSHA.

2Chama cha viziwi Tanzania (CHAVITA)kimeitaka serikali  kuitumia sheria  iliyotungwa na bunge kwa kutambua huduma muhimu za jamii hiyo ikiwemo  kuweka lugha ya alama katika mitaala ya kufundishia na kuajiri wakalimani kwenye vipindi vya luninga ya taifa ili waweze kupata huduma stahiki.
Kauli hiyo imetolewa na chama hicho cha viziwi kwa risala iyosomwa na Malisa Swila mwakilishi wa Chavita kwenye kilele cha wiki ya viziwi iliyofanyika kitaifa jijini hapa na kuwataka kutambua kuwa jamii hiyo 

inamchango sawa na jamii zingine katika taifa hili.
Swila alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ‘mtambuko wa viziwi katika jamii ‘lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano ya viziwi na jamii inayowazunguka kwa kupaaza sauti zao kupata stahiki zao na kutambuliwa katika jamii ikiwemo kupata huduma na kujikwamua kiuchumi.


“Sote tunajua Umuhimu wa lugha ya Alama kama lugha ya mawasiliano hivyo tunaiomba serikali kuiangalia na kuitambua lugha hiyo kwenye maeneo yote ya kutoa huduma za kijamii ikiwemo kuweka katika mitaala ya kufundishia kwenye mashule yetu hapa nchini”alisema Swila.
Akizungumza katika kilele hicho cha wiki ya viziwi hapa nchini Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa ArushaMagessa Mulongo alisema kuwa ujumbe wa chavita umefika kwa kutambua jamii hiyo inamchango katika maendeleo ya taifa.
Alisema kuwa kauli mbiu ina ujumbe muhimu sana kwa serikali kuchambua uanuai na umuhimu wa jamii hiyo kwa maendeleo ya taifa letu,ikiwemo lugha ya alama kutumika kwenye luninga na vyombo vya habari kuajiri wakalimani watakaosaidia jamii hiyo kupata kutoa maelezo yao pindi wanapotaka kufanya hivyo kwa manufaa ya jamii kwani hata wao wanamchango itakayoweza kuisaidia serikali na jamii.
Munasa alisema kuwa amesoma mabando yote yaliopo kwenye sherehe hizo licha ya maandamano yenu kuzuiwa kwa sababu za kiusalama,hivyo ujumbe umefika kwani kama wiki hii ilivyo kwenu ni kupata wasaa wa kuziangalia changamoto zenu mnazokutana nazo na kuzifikisha kwa watoa maamuzi,wanasiasa,wazazi na jamii kutambua mahitaji yenu.
“Lugha ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya taifa na watu wake,bila ya lugha hakuna mwasiliano hivyo bila ya kuwepo lugha ya Alama kwenu ni kukosa fursa na kupishana nazo hivyo tunaowajibu kama jamii kuitambua lugha hiyo ya alama kwa mustakabali wenu wa maisha”alisema Munasa.
Mkurungenzi wa jiji la Arusha alisema anatoa ahadi ya kulipia huduma za afya kwa viziwi 30 na kuwa atagharikia usafiri kwa wanachama wawili wa jumuiya hiyo kwenda popote katika maadhimisho ya CHAVITA hapa nchini.
Iddy alisema kwa jamii hiyo pia inamchango katika maendeleo ya jiji ndio maana jiji kwa kutambua hilo wakajikwamua kwa kutoa ahadi kama hizo ilikuweza kuwapa ushirikiano wa karibu kwa maendeleo ya taifa letu na jiji kwa ujumla huku akipongeza sherehe hizo kufanyika jijini hapa.
Naye mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Childreach ambao walikuwa wadhamini wa sherehe hizo alisema kuwa Sheila Mukhtary alisema kuwa shirika hilo limefanikiwa kwa kuto elimu kwa jamii hiyo kwa shule tatu zilizopo mkoani Kilimanjaro ikiwemo shule ya sekondani ya ufundi na shule za msingi mbili.
Alisema kuwa kukosekana kwa lugha za alama katika huduma za Afya kunapelekea jamii hiyo kutopata huduma stahiki hivyo akaimba serekali kutambua hilo na kuliweka katika mikakati yake.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya CHAVITA hapa nchini Hashimu Ismail aliwataka viongozi wakuu wa serikali akiwemo rais wa jamhuri ya muungano,makamu wake,waziri mkuu kuipa umuhimu wki ya viziwi kwa kushiriki maadhimisho yao kwani wamekuwa wakiomba wawe wageni rasmi kwa muda sasa bila ya mafanikio.

No comments:

Post a Comment