Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago
Bernabeu
umeisha kwa matokeo ya ushindi mzito kwa Real Madrid walioibamiza Basle 5-1.
Suchy alianza kujifunga goli kwenye dakika ya 14 na kuipa
uongozi Madrid, kabla ya Gareth Bale kufungua ukurasa wake wa magoli kwenye UCL
kwa kufunga goli la dakika ya 30, Cristiano Ronaldo akaongeza lingine dakika ya
31, James Rodriguez akafunga goli la 4 dakika ya 36, na Karim Benzema
akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la FC Basle dakika ya 79.
No comments:
Post a Comment