Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 24, 2014

Ajidai kuwa kwenye 'Coma' kwa miaka 2

 Alan Knighty alijidai kuwa mgonjwa mahututi ingawa alikamatwa na madaktari akiwa anajilisha
Mwanamume mmoja alitumia udanganyifu na kujidai kuwa mgonjwa mahututi kwa miaka miwili nchini Uingereza.
Alan Knight, mwenye umri wa miaka 47, kutoka mtaa wa Swansea, alimuibia mzee mmoja jirani yake pauni elfu arobaini kwa njia ya udanganyifu na kudai kuwa hengeweza kutembea kutokana na kupooza kutoka shingoni hadi miguuni.
Hii ilikuwa njama yake ili asiweze kukamatwa kwa kosa hilo. Inaarifiwa laikwepa polisi mara mbili kwani wakati hupo yeye mwenyewe alijipeleka hospitani ili asikamatwe na kushitakiwa.
 Kila wakati polisin walipotaka kumfikisha mahakamani , Knight alijipeleka hospitalini akidai kuwa hali yake imekuwa mbaya zaidi.



Hata hivyo siku zake za mwizi kushikwa zilifika pale wauguzi walipompata katika chumba chake hospitalini akiwa anakula , kupanguza mdomo wake na hata kuandika.
Kwa miaka miwili, Night alikwepa mkono wa sheria kwa kudai kuwa alikuwa hawezi kuamka wala kutembea na pia alikuwa tayari na uraibu wa kutumia gesi ya oxygen kama mtu ambaye hawezi kupumua bila usaidizi wa gesi hiyo.
Yote hayo yalikuwa ongo na ambayo yangewezekana tu kwa sinema.
 Alan Knight katika duka la Tesco, alinaswa na polisi kwa camera ya CCTV akisukuma gari la kubebea bidhaa ndani ya duka hilo wakati akidai kuwa mgonjwa mahututi.
Afisaa mmoja wa polisi Paul Harry,kutoka South Wales alisema: ‘Katika kazi yangu hii, sijawahi kuona kisa kama hicho ambacho kilipangwa na kutekelezwa kwa umaakini huo.''
Mkewe mwanamume huyo mwenye watoto watatu , pia alikuwemo kwenye sakata kwani siku zote alionekane akimhudumia mumewe aliyejidai kuwa hali mahututi. T
Mbunge wa eneo la Swansea West aliambia BBC kuwa: "Nilikutana na Bi Hellen na akaniarufu ambavyo mumewe alikuwa na hali mbaya ya kiafya na kwamba walitendewa vibaya na polisi.''

Knight anakabiliwa na mashitaka 19 ikwemo wizi na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela.

No comments:

Post a Comment