Manchester United msimu huu imejaribu kujiimarisha katika idara ya ushambuliaji kwa kufanya usajili wa kuvunja rekodi nchini Uingereza wakiwa na nia ya kutaka kurejesha makali yao yaliyopotea msimu uliopita lakini uwepo wa majeruhi takribani tisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu hao kinaifanya klabu hiyo kuweweseka.
Hivi karibuni klabu hiyo imetokea kumuamini mlinzi kinda Paddy McNair aliyekuwa akishirikiana vyema na Muajentina Marcos Rojo katika kuimalisha ulinzi wa katikati wa klabu hiyo lakini katika kile
kinachoonekana kama kuandamwa na jinamizi la mkosi wa majeruhi kijana huyu naye amelipotiwa kupata maumivu ya misuli daraja la tatu aliyoyapata siku ya Jumapili wakati timu yake ya Manchester United ilipokipiga dhidi ya Everton na kupata ushindi wa magoli 2:1.

Kuumia kwa McNair kunatimiza idadi ya walinzi watano wa wa klabu ya Manchester United wanaokaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambapo wengine ni Luke Shaw (kifundo cha mguu), Jonny Evans (kifundo cha mguu), Phil Jones (misuli) na Chris Smalling (nyama za paja).
No comments:
Post a Comment