Kahawa hiyo huuzwa kati ya dola za kimarekani 3 hadi 5 kwa
kifuko kidogo kinachotosha kikombe kimoja cha chai, na bei hiyo itategemea
jinsi wewe ulivyo mtaalamu wa kuomba punguzo la bei inaweza kushuka.
Wachuuzi hao wa mitaa ya Harare wamezungumza na kudai kuwa
kahawa hiyo huwasaidia wanaume kupata hamu ya kufanya ngono kwa muda mrefu
Zaidi,lakini pia humchelewesha mwanaume kupata mshindo kwa muujibu wa utafiti
wao.
Pindi tu uinunuapo kahawa hiyo,wachuuzi hao hukupa maelekezo
kuwa uinywe dakika 15 kabla ya tukio lenyewe na humpa nguvu mtumiaji ya kufanya
ngono kwa saa sabini na mbili,ingawa madai hayo hayajathibitishwa kitabibu.
Wanaume wengi inaarifiwa wamechangamkia sana kahawa hio yenye vijimambo
Wachuuzi hao wameamua kufanya biashara yao katika mtindo wa aina yake,kwa kuiuza kahawa hiyo katika maeneo maarufu nchini Zimbabwe yenye mikusanyiko ya watu kama eneo la KwaMereki kwenye viunga vya bustani ya kitongoji cha Warren, Zindoga eneo lililoko kwenye maporomoko ya maji (Waterfalls) na eneo la vilima la KuHuku .
Kitu cha kuvutia biashara hiyo hufanywa na wachuuzi wa kike wafanyao kazi katika duka kubwa la
Fife Avenue Shopping centre wenye kutoa ushuhuda na kukubali kuwa waume zao waliitumia kahawa hiyo na wakayaona matokeo yake nao wakafaidi kwani uwezo wao uliongezeka maradufu.
Ingawa wanawake hao pamoja na kukubali na kutoa ushuhuda huo, bado hawako tayari kuelezea wapi wanakozinunua kahawa hizo za majamboz na kwa sasa mjini Harare mahitaji ya kahawa hiyo ni makubwa mno na ni rahisi kuitumia kwani unaweza kuitumia kwa maji moto ama baridi anaeleza muuzaji aliyejitaja kwa jina moja la Anna.
Anna anasema wateja wake wakubwa ni waume kwa wake ingawa wanawake wana aibu kuinunua kahawa hiyo hadharani kuliko wanaume wao hawana aibu pindi wanapotaka kahawa hiyo kwa matokeo mazuri ya kulinda heshima shughulini.
Kwa muujibu wa daktari mmoja nchini Zimbabwe aliyekataa kutajwa jina lake amesema kwamba tatizo la nguvu za kiume nchini Zimbabwe ni kubwa mno kwa wanaume walio wengi na linakua siku hadi siku na kusema ni tatizo kubwa.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment