Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limetoa orodha ya nchi
zilizojitokeza kuwania kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Nchi saba wanachama zimewasilisha maombi hayo kabla ya tarehe ya mwisho
iliyowekwa ya Septemba 30 2014.
Nchi hizo ni Algeria, Misri, Gabon, Ghana, Kenya, Sudan na Zimbabwe.
Nafasi ya kuandaa michuano hiyo ya 31 ilitolewa Agosti 23
2014, kufuatia Libya kujiondoa.
No comments:
Post a Comment