Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 25, 2014

JUMA NATURE AFUNGUKA KUHUSU WASANII KUNUNUA MASHABIKI

Juma Nature
Leo ndo siku ambayo aliyekua msanii wa kundi la Wanaume Family ‘YP’ amezikwa ikiwa imepita siku moja tu tangu afariki dunia. Chanzo cha kifo cha msanii huyo ni ugonjwa wa kifua ambao ulikua ukimsumbua kwa mda mrefu. Bongoclan ilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Juma Nature ambapo alisema ni huzuni kubwa sana kumpoteza

 msanii mwenzake ambaye walikua wakifanya kazi pamoja tangu zamani.

Pia tuliweza kumuuliza ni kitu gani anajivunia kuhusu mziki wake na alikua na haya ya kusema ” Mimi najivunia nina mashabiki wengi kuliko mtu yeyote Tanzania, nina mashabiki wengi sana ambao hawana fitna na sio wa kutengenezwa. Wanaotengeneza mashabiki huo ni ulimbukeni kwa sababu labda ni tamaaa za pesa, kuna mtu mwingine anataka kutengeneza kitu labda anataka kua mtu flani kwa kuforce. Mziki tuliokua tunafanya sisi sio wa kutengeneza kama mtu anaomba nyimbo yako redion anaomba sio kwamba msanii kamwambia piga simu uombe nyimbo yangu redion. Sasa athari zake tutakosa msanii bora ambaye ataiwakilisha Tanzania au hata Afrka.


Habari imeandikwa na Eddie Sucre na Sweetbert Abednego wa Zenji Fm

No comments:

Post a Comment