Waswahili husema mtu hasahau asili.
Barani Afrika kuna mimea mbalimbali ambayo bado inatumika
kwa ajili ya matibabu, licha ya mingine mingi kutumika kama chakula.
Hivi karibuni, mwandishi wetu Zuhura Yunus alikuwa mkoani
Kigoma nchini Tanzania. Katika pita pita yake alikutana na mmea ambao awali,
kwa kuutazama alidhania ni mbuyu.
Hata hivyo, alipozungumza na wenyeji wa eneo hilo
linalojulikana kama Kabwe, akaelezwa mmea huo unaitwa Mlemela. Nini kilimvutia
mwandishi wetu hata kuufuatilia mmea huo?
Zuhura alifanya mahojiano na mkazi wa Kigoma, Birangwa Musa
ambaye alimueleza kuwa mmea huo unatumika kwa matibabu hasa kwa wanaume.
Kwanini wanaume?
No comments:
Post a Comment