Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg
amenunua sehemu kubwa ya kisiwa cha Hawaii iitwayo Kauai ambayo ni hekari 700
kwa dola za Kimarekani milioni 100 ambapo atakuwa anamiliki eneo kubwa ambalo
litaendana na hadhi ya bilionea, jarida la Forbes limeripoti.
Hekari hizo 700 zitajumuisha beach resort, mashamba ya miwa
na kilimo hai ambapo kwa sheria za Hawaii beach resort hiyo lazima iachwe wazi
kwa matumizi ya jamii kwa sababu kisiwa hiko hakina sheria ya umiliki binafsi
wa mchanga.
Mwaka jana mwenyekiti wa Oracle Larry Ellison alinunua
upande mzima wa Lanai, Hawaii kwa dola milioni 600 ambapo stori nyingine zinasema Zuckerbug nae anaweza akawa na nia
ya kuanzisha
majengo upande huo wa Lanai baada ya kuonekana na mkewe Priscilla
Chan kwenye maeneo hayo.
Haya yatakua maendeleo mengine ya Zuckerberg kwani mwaka
2010 alikodisha jengo lake ambalo lipo karibu na makao makuu ya office za Faceboook na mwaka uliofata
aliongeza makazi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 7 huko Palo Alto,
California, Marekani ambapo pia baada ya muda mfupi alitumia dola milioni 30
kununua nyumba nne ambazo ziliunganishwa na makazi yake ya Palo Alto.
Alivyoulizwa kuhusu ripoti zilizotolewa hivi karibuni kuhusu
matumizi yake ya pesa msemaji wa Facebook alisema ‘Hatuna chochote cha kusema
kuhusu maneno ambayo hayana ukweli ila asante kwa kututafuta’
No comments:
Post a Comment